Home Uncategorized SPURS YAHAHA KUMBAKIZA KANE NDANI YA KIKOSI

SPURS YAHAHA KUMBAKIZA KANE NDANI YA KIKOSI

HARRY Kane nyota wa timu ya Spurs inaelezwa kuwa yupo kwenye hesabu za kusepa ndani ya klabu hiyo kwenye majira ya joto.

Mabosi wa timu hiyo wakiongozwa na Kocha Mkuu, Jose Mourinho wameanza hesabu za kuongea naye ili kumshawishi abaki ndani ya kikosi hicho.

Spurs inaamini kuwa nyota huyo mwenye miaka 26 ana uwezo mkubwa na thamani yake inahitajika ndani ya kikosi hicho kutokana na kazi kubwa anayoifanya.

Taarifa zinaeleza kuwa nyota huyo anahitaji pauni milioni 150 ili kupata saini ya nyota huyo na mabosi wapo tayari kumpa mkwanja wote.

SOMA NA HII  UNAAMBIWA GSM BABA LAOO..WARUDI YANGA KWA SPIDI 360..!!