SINGIDA United jana iliambulia kichapo cha mabao 8-0 mbele ya Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Uhuru.
Mchezo huo ulishuhudia mabao mengi kwa msimu wa 20219/20 kufungwa kwa timu moja huku Singida United ikimaliza ikiwa pungufu kwa wachezaji 10 baada ya kiungo wao mkongwe, Haruna Moshi ‘Boban’ kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 54 kwa kile alichoonekana akimpiga kiwiko mlinda mlango wa Simba Aishi Manula.
Kutoka kwa Boban kulivuruga mipango ya wachezaji wenzake ambao walishindwa kupata bao la kufutia machozi kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Uhuru.
Kichapo hicho kinakuwa cha 20 kwa Singida United iliyo nafasi ya 20 baada ya kucheza mechi 28.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.