RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia ameelekeza Kamati ya Uongozi ya Bodi ya Ligi Kuu kuitisha kikao cha dharura kesho Machi 18,2020,
Kikao hicho kinatarajiwa kufanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, Dar majira ya saa 3:00 asubuhi.
Ajenda kubwa kwenye mkutano huo ni kujadili mustakabali wa Ligi Kuu Bara kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Corona ambao umeingia nchini.






