Home Uncategorized KUBETI KWAMPONZA STURRIDGE, FA, FA ZAMFUNGIA, KLABU YAKE YAMTEMA

KUBETI KWAMPONZA STURRIDGE, FA, FA ZAMFUNGIA, KLABU YAKE YAMTEMA





Klabu ya Trabzonspor ya Uturuki imemtema mshambuliaji wake, Daniel Sturridge.

Sturridge ambaye ni mshambuliaji wa zamani wa Chelsea na Liverpool, ametemwa baada ya kubainika ndugu yake acheze kamari wakati yeye akiunga na timu hiyo.
Ndugu yake huyo ambaye imeelezwa ni kaka yake, alicheza kamari na kushinda mamilioni ya fedha akitabiri yeye Sturridge atajiunga na klabu hiyo ya Uturuki.

Adhabu ya Trabzonspor, inafuatia adhabu ya FA na Fifa ambazo zimemfungia hadi Juni kutokana na kittende hicho.

Kawaida Fifa, FA na mashirikisho mengine ya soka yanazuia wanasoka kushiriki kwa aina yoyote katika masuala ya kamari.

Awali Sturridge alikata rufaa lakini akashindwa mara nyingine.
SOMA NA HII  KAGERA SUGAR YAMUIBUA HAJI MANARA KWA FUJO, ATOA TAMKO ZITO JUU YA YANGA