Home Uncategorized KUMBE MABEKI SIMBA WALIKAMIA MCHEZO WAO MBELE YA YANGA, MSHAMBULIAJI ALIYEWAPA TABU...

KUMBE MABEKI SIMBA WALIKAMIA MCHEZO WAO MBELE YA YANGA, MSHAMBULIAJI ALIYEWAPA TABU ASIMULIA

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Ditram Nchimbi amesema kuwa miongoni mwa sababu zilizoifanya timu yake kusepa na pointi tatu mbele ya Simba Machi 8 Uwanja wa Taifa ni kukamia kwa mabeki wa Simba mchezo huo mwanzo mwisho.

Nchimbi alikuwa msumbufu kwenye mchezo huo ambapo licha ya kushindwa kufunga aliwachosha mabeki wa Simba waliokuwa wakimkaba kwa zamu ambapo aliwekwa kwenye uangalizi mkubwa na Pascal Wawa.

Nchimbi amesema: “Mabeki wa Simba walipania mchezo tangu tunaanza walikuwa wanaamini kwamba tutawaogopa jambo ambalo halikutokea na mwisho wa siku wakapoteza nasi tukashinda.

“Pascal Wawa alikuwa anaamini kwamba nitaingia uwanjani nikiwa na hasira kwa kuwa alinichezea rafu kwenye mchezo wetu uliopita kumbe mimi nilikuwa nimesahau na nilingia nikiwa na kazi moja ya kuipa timu matokeo.

“Hasira za mabeki wao ziliwaponza ila kidogo Erasto Nyoni alikuwa anatumia akili tofauti na Wawa ambaye alikuwa anatumia nguvu hilo lilitupa nguvu,” amesema.

Mchezo wa kwanza Yanga ikiwa ugenini ililazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 Januari 4 Uwanja wa Taifa na mchezo wa pili Yanga ilisepa na pointi tatu kwa ushindi wa bao 1-0.

SOMA NA HII  KUPOTEZA KWA KUCHAPWA NA BURUNDI NYUMBANI IWE SOMO KWA STARS