Home Uncategorized STAA WA SIMBA ATANGULIA MBELE ZA HAKI, SIMBA YAMLILIA

STAA WA SIMBA ATANGULIA MBELE ZA HAKI, SIMBA YAMLILIA


DAMIAN Mrisho Kimti aliyekuwa mchezaji wa zamani wa Simba amefariki dunia Jana jioni, Machi 2.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na uongozi wa Simba imeeleza kuwa Kimti alikuwa miongoni mwa wachezaji waliocheza mchezo wa Fainali ya Ligi ya Ubingwa Afrika Mashariki 1992 pia alicheza mechi ya Fainali ya Kombe la CAF 1993 dhidi ya Stella Abidjan.


Aliyekuwa Mwenyekiti wa Simba, Hassan Dalali amesema kuwa amepokea taarifa hizo kwa mshtuko kutokana na ukaribu wake na mchezaji huyo ambaye alikuwa kipenzi cha mashabiki kutokana na kuwa na uwezo mkubwa wa kufunga.

Msiba wa nyota huo upo nyumbani kwakwe Kimara.

SOMA NA HII  WAWILI WAONDOKA YANGA