Uncategorized

NIYONZIMA AGOMEA KUSTAAFU KUCHEZA SOKA

admin April 3, 2020 6:14 am

HARUNA Niyonzima, kiungo mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa kwa sasa hana mpango wa kustaafu kucheza mpira kutokana na uwezo wake alionao ndani ya uwanja.

Niyonzima amesema kuwa bado anajua anahitajika ndani ya uwanja kwani uwezo na ujuzi unadumu.

“Kwa sasa sina mpango wa kustaafu kucheza soka kwa sasa nitaendelea kupambana ili kuwa bora na kufanya vizuri ndani ya uwanja.

“Wapo wanaotaka itokee hivyo kwangu lakini bado sijafikiria mpaka wakati utakapofika nitaamua kufanya hivyo ila sio kwa sasa,” amesema. 

MUONEKANO WA UKURASA WA NYUMA GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA ABDI BANDA: TUNAPIGA MATIZI KAMA KAWAIDA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply