BEKI wa zamani wa kikosi cha Arsenal, Bacary Sagna amesema kuwa klabu hiyo itafanya makosa makubwa iwapo itamuuza nahodha wao, Pierre-Emerick Aubameyang.
Nahodha wa Arsenal Auba amekuwa akihusishwa kusepa ndani ya Arsenal msimu huu huku ikielezwa kuwa amekuwa hana furaha ndani ya timu hiyo kwa kuwa haishiriki kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Dili la Aubameyang limebakiza miezi 12 ndani ya Emirates na inaelezwa kuwa tayari mabosi wa Klabu ya Arsenal wameanza kuzungumza naye ili kumuongezea mkataba wake mpya.
Sagna amesema Arsenal itafanya
makosa makubwa iwapo itamuuza mchezaji huyo kwani amekuwa kwenye ubora wake na anafanya makubwa kwa ajili ya timu yake.
“Iwapo watazubaa ana nafasi kubwa ya kuondoka kwa sasa ndani ya Arsenal kutokana na juhudi zake alizonazo na itakuwa ni makosa makubwa kwao kumruhusu nyota huyo aondoke ndani ya klabu.
“Anastahili kubaki ndani ya kikosi licha ya kuonekana ana uwezo wa kufunga basi wanapaswa wajifunze kupitia makosa ambayo waliwahi kuyafanya nyuma kwa kuwaacha wachezaji wao kipindi cha nyuma,” amesema.