EDINSON Cavani anamatumaini ya kucheza La Liga katika msimu ujao wa ligi, hii baada ya dirisha lililopita la Januari kukwama.
Atletico ilikuwa mbioni kukamilisha usajili wa staa huyo kipindi cha Januari, lakini inaoneka PSG kuweka ngumu japo alikuwa amesalia na miezi sita.
Cavani mkataba wake unamalizika Juni 30, mwaka huu na sasa ataondoka kama mchezaji huru ndani ya klabu yake hiyo ambayo alidumu kwa muda mrefu.
Kocha Atletico Madrid, Diego Simeone amekuwa akihitaji nguvu katika safu yake ya ushambuliaji na amekuwa akimuhitaji Cavani kwa muda mrefu.
Huenda msimu ujao, straika huyo akavalia uzi wa Atletico endapo mambo yatakwenda sawa ingawa Atletico bado inamatumaini ya kumpata.
Hata hivyo, Rais wa Atletico, Enrique Cerezo alifunguka kuhusu dili la Cavani: “ Wakati mwingine kwenye usajili wale ambao wanasimamiwa na familia kuna kuwa na tatizo mara nyingine.
Cavani katika masuala ya usajili amekuwa akisimamiwa na kaka yake pamoja na baba yake na usajili uliopita walihusika zaidi.
Kuelekea msimu ujao, licha ya Cavani kutajwa kujiunga na Atletico, lakini amekuwa akihusishwa na klabu za Napoli, Man United na hata Chelsea.