Home Uncategorized KMC WAVUNJA KAMBI, WACHEZAJI WANAFUTILIWA KWENYE MITANDAO

KMC WAVUNJA KAMBI, WACHEZAJI WANAFUTILIWA KWENYE MITANDAO


UONGOZI wa KMC umesema kuwa unawafuatilia wachezaji wao namna wanavyofanya mazoezi kupitia makundi ya WhatsApp jambo ambalo linawafanya wazidi kufanya mazoezi zaidi.
Ligi Kuu Bara iliposimamishwa wachezaji wa KMC iliripotiwa kuwa wapo kambini na wanaendelea na mazoezi ila kwa sasa uongozi umesema kuwa umevunja kambi na kila mchezaji anaendelea na mazoezi nyumbani.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Ofisa Habari wa KMC, Anwary Binde alisema kuwa wachezaji wapo nyumbani na wamepewa program ya kufanya.
“Wachezaji wapo nyumbani kwa sasa wanaendelea na mazoezi ambapo tunawafuatilia kupitia magroup yetu ya WhatsApp huko ndiko ambapo benchi la ufundi linatoa taarifa za maendeleo yao pamoja na kuwapa mazoezi mengine,” alisema Binde.
SOMA NA HII  MUONEKANO WA KAMBI MPYA YA YANGA 2020/21