KIPA wa zamani wa Simba, Ally Mustapha ‘Barthez’ amebainisha kuwa hata nafasi ya beki wa kati anacheza freshi tu lakini akaonyesha Simba hii ni balaa.
“Ile safu ya ushambuliaji ya Simba hatari sana, tulipata shida sana tulipokutana nao. Ogopa sana timu ambayo kila mchezaji anaweza kufunga, ndivyo ilivyo kwa Simba, safu yao ya ushambuliaji muda wowote inakufunga,” alisema Barthez.
Alisema kwamba mwaka 1999 wakati akiwa Shule ya Msingi Karakata iliyopo Uwanja wa Ndege, Dar es Salaam alikuwa akicheza kama beki wa kati, lakini siku moja kukawa na uhaba wa kipa kwenye timu yao ndipo akapangwa yeye na ndio safari ya kuwa kipa mahiri ilipoanzia.
“Nilikuwa beki wa kati nafasi ambayo hata sasa hivi naweza kucheza vizuri kabisa lakini chanzo cha kuhamia kuwa kipa ilianzia shuleni kwani kila makipa walipokosekana nilikuwa naambiwa nidake, hivyo nikazidi kuzoea mpaka leo ndio hiyo nafasi ninayocheza mpaka sasa,” alisema Barthez ambaye kwa sasa anakipiga Ndanda FC ya Mtwara.