Home Uncategorized NIYONZIMA: AFYA NI MUHIMU, TUCHUKUE TAHADHARI

NIYONZIMA: AFYA NI MUHIMU, TUCHUKUE TAHADHARI

HARUNA Niyonzima, kiungo mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa ni muhimu kwa kila mmoja kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona ili kuwa salama.

Kwa sasa Ligi Kuu Tanzania Bara imesimamishwa kwa muda ili kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona.

Akizungumza na Saleh Jembe, Niyonzima amesema kuwa kuna mambo mengi kwa sasa yamesimama ila ni muhimu kuzingatia afya kwanza kisha mengine yatafuata.

“Muhimu kuzingatia kanuni za afya na kufuata kanuni ili kuwa salama, kuna mengi ambayo yamesimama kwa sasa lakini afya ni muhimu kwa kila mmoja,” amesema.

SOMA NA HII  MASTAA HAWA UANGA WAITAMANI SIMBA KUFA KUPONA DABI YA KARIAKOO