BEKI wa Polisi Tanzania, Luccian William, ‘Gallas’ amesema kuwa kwa sasa anaendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona huku akiwaomba watanzania kufuata kanuni za afya.
Akizungumza na Saleh Jembe, Gallas amesema kuwa kwa sasa kila mmoja ni lazima azingatie kanuni za afya ili kujilinda na Virusi vya Corona.
“Kwa sasa kila mmoja ni lazima achukue tahadhari ya kujilinda dhidi ya Virusi vya Corona kwani vipo na vinasambaa pia hapa Bongo.
“Kikubwa cha kufanya ni kufuata kanuni zilizowekwa na Wizara ya afya pamoja na Serikali ili kila mmoja awe salama,” amesema.