IBRAHIM Ajibu, kiungo mshambuliaji ndani ya Simba amesema kuwa wakati huu wa mapumziko ya Ligi Kuu Bara kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona amekuwa akichukua tahadhari huku akifanya mazoezi kulinda kipaji chake na kujitoa kwa jamii.
Ajibu amesema kuwa amekuwa akitoa misaada kwa jamii ili kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kupambana na maambukizi ya Virusi vya Corona.
“Nimekuwa nikifanya mazoezi ili kulinda kipaji changu kwani kwa sasa ligi imesimama na hakuna ambacho kinaendelea zaidi ya mazoezi binafsi ambayo kila mmoja anapaswa kufanya.
“Pia nimekuwa nikitoa misaada kwa jamii ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Serikali kupambana na Virusi vya Corona nami nimekuwa nikichukua tahadhari kwa kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima,” amesema.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.