Uncategorized

ISHU YA YANGA KUSHUSHA PANCHA MOJA MATATA UONGOZI WAFUNGUKA, WAKIRI KUWAFUATILIA KWA UKARIBU

admin April 20, 2020 8:29 am

UONGOZI wa Yanga umesema kuwa unawafuatilia kwa karibu nyota wote wanaokipiga ndani ya Ligi Kuu Bara ili waweze kuona namna gani wanaweza kuzipata saini zao ikiwa ni pamoja na Relliats Lusajo na Lukas Kikoti.

Miongoni mwa nyota ambao wanafuatiliwa kwa ukaribu na Yanga ni pamoja na pacha hiyo ya Namungo ambayo imekuwa na muunganiko mzuri.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa Klabu ya Yanga inazifuatilia timu zote ndani ya Bongo ili kuona inapata wachezaji wazuri.

“Yanga inafuatilia wachezaji wote ndani ya Ligi Kuu Bara ili kuona namna gani inaweza kupata saini zao kwani kila timu inahitaji wachezaji makini.

“Kuhusu kupata saini zao kwa sasa hao akina Lusajo, Kikoti ni tetesi tu ila wakati wa usajili ukifika tunaweza kuzungumzia hilo ila kuwafuatilia wachezaji ni jambo la kawaida kwa sasa,” amesema.

BEKI SIMBA AWAOMBA WATANZANIA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA CORONA LONGSTAFF AWEKWA KWENYE HESABU ZA AC MILAN ATAJA MASHARTI YA KUWAGA WINO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply