Uncategorized

UWEZO WA KAPOMBE WAMVUTIA BEKI HUYU ANAYEKIPIGA KCB, ATAKA KUJA SIMBA

admin April 21, 2020 1:29 pm

SIMBA ishindwe yenyewe kwa beki wa kati wa timu ya taifa ya Kenya na Klabu ya KCB ya nchini humo, Michael Kibwage ambaye amesema anatamani kucheza pamoja na beki Shomari Kapombe huku akisema yupo tayari kujiunga nayo msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
Simba ipo kwenye mipango ya kuifumua safu ya ulinzi ya timu hiyo kwa kusajili mabeki wa kati wenye viwango vikubwa.
Kwa mujibu wa mtandao mmoja wa Kenya, beki huyo kwa muda mrefu ameonekana kuvutiwa na aina ya uchezaji wa Kapombe katika nafasi ya beki ya kulia.

 Kibwage alisema anaamini siku moja atakutana na kucheza pamoja katika timu moja kama siyo Simba, basi kwingine.
“Nchini Tanzania navutiwa sana na aina ya uchezaji ya Kapombe, kwangu ni kati ya mabeki bora katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
“Ni beki wa kulia anayefanya majukumu yake vizuri ikiwemo kulinda goli lake na kuanzisha mashambulizi kupitia upande wake wa kulia,” amesema.
TSHISHMIBI NA FEI TOTO WAMVUTA NDANI YA YANGA KIUNGO MKALI WA KENYA TEGETE AWAOMBA WATANZANIA KUENDELEA KUCHUKUA TAHADHARI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply