Uncategorized

TSHISHMIBI NA FEI TOTO WAMVUTA NDANI YA YANGA KIUNGO MKALI WA KENYA

admin April 21, 2020 12:59 pm



YIDAH Sven, kiungo anayekipiga ndani ya Klabu ya Kariobang Sharks ya Kenya amesema kuwa anavutiwa na uwezo wa kiungo Papy Tshishimbi na Fei Toto ambao wanakipiga Yanga jambo ambalo litampendeza akiungana nao.

Sven alipata nafasi ya kucheza na wachezaji hao kwenye mchezo wa siku ya Wanachi Uwanja wa Taifa ambapo ulikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

Kwa sasa inaelezwa kuwa mabosi wa Yanga wanaiwinda saini ya kiungo huyo ambaye anakaribia kumaliza mkataba wake ndani ya Sharks.

Sven amesema:”Nipo tayari kutua ndani ya Klabu ya Yanga kwani ni timu kubwa ambayo kila mmoja atapenda kucheza bila mashaka yoyote.

“Ninawatambua baadhi ya viungo wanaokipiga Yanga ikiwa ni pamoja na Fei na Tshishimbi hawa wapo vizuri nitafurahi iwapo nitapata nafasi ya kucheza nao,” .
BOGA AYAKUMBUKA MAISHA YA CHELSEA UWEZO WA KAPOMBE WAMVUTIA BEKI HUYU ANAYEKIPIGA KCB, ATAKA KUJA SIMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply