KIUNGO wa Borussia Dortmund, Emre Can amefunguka kuwa aliyewahi kuwa kocha wake Maurizio Sarri alishindwa kumpa nafasi, lakini kwa kiasi alipata uzoefu.
Can amejiunga na Dortmund katika usajili wa dirisha dogo wa Januari akitokea Juventus ambako alikuwa hana nafasi kwenye kikosi cha Sarri.
Kiungo huyo kilichomkimbiza zaidi Juventus ni kile kitendo cha kuachwa katika kikosi cha wachezaji ambao walikuwa wanashiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.
Can alisema: “Sarri hakutaka kunipa nafasi ndani ya Juventus, nimepitia nyakati ngumu sana nikiwa pale na kocha yule.
“Nilikuwa mchezaji muhimu na bora mwaka mmoja kabla na baada ya kutwaa tajin kwa kucheza vizuri michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
“Lakini pamoja na yote, Juventus kwangu inabaki kuwa sehemu nzuri na yenye kumbukumbu nzuri katika kazi yangu,”alisema Can.
Kiungo huyo alijiunga na Juventus akiwa mchezaji huru kutoka Liverpool mwaka 2018 na akiwa hapo alicheza mechi 45 kufunga mabao manne na kutoa asisti moja.