Home Uncategorized KIUNGO MKANDALA AZICHONGANISHA AZAM NA NAMUNGO

KIUNGO MKANDALA AZICHONGANISHA AZAM NA NAMUNGO

AZAM FC na Klabu ya Namungo zipo kwenye hesabu za kuinasa saini ya kiungo Cleophance Mkandala anayekipiga ndani ya Tanzania Prisons.

Kiungo huyo amekuwa kwenye ubora wake msimu huu ambapo ametoa jumla ya pasi nne za mabao kwenye klabu

yake.

Habari zinaeleza kuwa Azam FC iliyo chini ya Kocha Mkuu Arstica Cioaba ina mpango wa kuboresha kikosi kwa ajili ya msimu ujao huku Namungo ikisaka mbadala wa Lukas Kikoti anayetajwa kuibukia Simba.

Kocha Mkuu wa Namungo, Hitimana Thiery amesema kuwa masuala ya usajili kwa sasa bado wakati wa kuzungumzia haujafika.

SOMA NA HII  MASHABIKI TUNAPASWA TUWE WASIKIVU, TUACHE UKOROFI NA KIBURI KATIKA KUFUATA MUONGOZO