UONGOZI wa Azam FC, umesema kuwa mpango mkubwa uliopo kwa sasa ni kujenga kikosi imara kwa ajili ya mashindano ya kitaifa na kimataifa kwa msimu ujao wa 2020/21.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Zaka Zakazi amesema kuwa bado kuna mipango inaendelea kupangwa na mingine inatimizwa taratibu kufikia malengo.
“Kufika malengo yalipo sio safari ya siku moja kuna mchakato ambao tunapitia kwa hatua ambayo tupo ni lazima tuwe na subira pamoja na hesabu kali kufikia mafanikio kitaifa na kimataifa kikubwa ni sapoti pamoja na dua,” amesema.
Azam FC iliyo chini ya Kocha Mkuu, Arstica Cioaba raia wa Romania na kapten wao akiwa ni Agrey Morris ipo nafasi ya pili Kwenye msimamo na kibindoni ina pointi 54 baada ya kucheza mechi 28.