Home Uncategorized MYWEATHER ATAJA SABABU ITAKAYOMRUDISHA ULINGONI, YEYE NI CHIZI SAA

MYWEATHER ATAJA SABABU ITAKAYOMRUDISHA ULINGONI, YEYE NI CHIZI SAA


FLOYD Mayweather, amesema kuwa licha ya kutangaza kustaafu kupanda ulingoni kuzichapa ila anaweza kurejea tena ikimbidi kufanya hivyo.

Bondia huyo ambaye alivuna mkwanja mrefu baada ya kumtwanga bondia Conor McGeorge 2017 ambapo inaelezwa kuwa alikunja pauni milioni 300 sawa na bilioni 855.

Mpambanaji huyo ambaye ni chizi saa akiwa anamiliki saa zaidi ya 41 huku moja ile iliyotengenezwa na Jacob & Co yenye thamani ya pauni milioni 14 ndiyo ya ghali zaidi.

“Kama nilivyosema mwanzo nimestaafu, lakini sijastaafu kutengeneza dola kadhaa,kama ninaweza kuiburudisha dunia na nikatengeneza dola milioni 600 kwa nini nisirudi ulingoni? “.

SOMA NA HII  YANGA YATUMA SALAMU HIZI KWA MBAO FC KESHO