Home Uncategorized OLE GUNNAR ANAAMINI RASHFORD NI MATATA KULIKO KANE

OLE GUNNAR ANAAMINI RASHFORD NI MATATA KULIKO KANE


OLE Gunnar Solskjaer, Kocha Mkuu wa Manchester United amesema kuwa ana furaha kwa kuwa klabu yake haikutumia pauni milioni 200 kuinasa saini ya Harry Kane.

Solskjaer amesema anaamini uwezo wa mshambuliaji wake Marcus Rashford kuwa ni bora kuliko Kane.

Imekuwa ikielezwa kuwa United inasaka saini ya Kane lakini dili hilo limekuwa likibuma.

Rashford yupo nyuma ya Kane kwa miaka minne lakini alikuwa mmoja kati ya wafungaji mahiri kwenye timu hiyo baada ya kufunga mabao 11 kabla ya kupata majeraha ya nyama za paja msimu huu.

SOMA NA HII  KIKOSI CHA YANGA DHIDI YA MTIBWA SUGAR