Home Uncategorized BEKI HUYU MZAWA AINGIA ANGA ZA SIMBA, KUKIPIGA NA KAPOMBE

BEKI HUYU MZAWA AINGIA ANGA ZA SIMBA, KUKIPIGA NA KAPOMBE

Kibwana Shomari, beki wa kulia wa Mtibwa Sugar inaelezwa kuwa yupo kwenye hesabu za Mabingwa watetezi Simba ambao wanaiwinda saini yake.

Simba ina hesabu za kubore

sha kikosi ili kukifanya kiwe cha kimataifa zaidi ambapo wanahitaji kuwa na wachezaji zaidi ya wawili kwenye nafasi moja.

Kutokana na uwezo wa Shomari wanaamini kuwa anafaa kusaidiana kazi pale Msimbazi na Shomari Kapombe ambaye amekuwa kwenye ubora wake msimu huu akiwa na pasi tano za mabao.

Thobias Kifaru, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar amesema kuwa kwa sasa sio wakati wa kukaa mezani kujadili ofa bali ni muda wa kupambana na Virusi vya Corona.

“Mtibwa tuna vipaji na tumekuwa chuo cha kuazalisha wachezaji,  kwa sasa hatuwezi kukaa chini kujadili ofa tunapaswa kupambana na Virusi vya Corona Kwanza kisha mengine yatafuata,” amesema.

SOMA NA HII  MAMBO 7 YANAYOILAZIMISHA ASTON VILLA KUHAKIKISHA INAMPATA NA KUMTUMIA SAMATTA