NAHODHA wa Yanga, Papy Tshishimbi amesema kuwa sababu kubwa inayomfanya awe tofauti kwenye mechi kubwa za kitaifa na kimataifa ni maamuzi yake kutumia uwezo wake wote ili kujiweka sokoni.
Tshishimbi amesema kuwa anaziamini mechi ngumu kuwa ni nafasi yake ya kutokea kwani hata Yanga walimsajili baada ya kumuona akicheza mechi za kimataifa.
“Tukikutana na timu ngumu ambazo ni mechi kubwa mfano Simba hapo huwa ninacheza tofauti na mechi nyingine kwa kuwa watu wengi wanazitazama mechi kubwa nami ni mchezaji ninajua ni muda wangu wa kujiweka sokoni.
“Haina maana kwamba mechi nyingine huwa zikazani hapana ni utofauti kidogo pale mnapokutana wote mnajua mpira na ni watu wakubwa lazima nawe ujiongeze ili kuwa bora, Yanga pia waliniona kwenye mashindano ya kimataifa hivyo naziheshimu mechi kubwa zina faida kwangu na timu pia,” amesema.
Yanga ikiwa imecheza mechi 27 ametumia dakika 1,936 akicheza mechi 23, ambapo mechi za kazi zote ngumu ambazo ni zile za timu ambazo zipo ndani ya tano bora Simba, Namungo,Azam FC na Coatal Union aliziyeyusha dakika zote 90 bila kuwekwa benchi.