Uncategorized

FAROUK SHIKALO AZUNGUMZIA HATMA YAKE NDANI YA YANGA

admin May 11, 2020 8:57 am


FAROUK Shikalo, mlinda mlango namba moja wa Klabu ya Yanga amesema kuwa hana mashaka iwapo atapigwa chini msimu ujao ndani ya kikosi hicho.

Nyota huyo raia wa Kenya anakipiga pia kwenye timu yake ya taifa ameshindwa kurejea Bongo kutokana na mipaka ya Kenya kufungwa sababu ya janga la Virusi vya Corona.

“Sina wasiwasi wowote na hilo kwani ni jambo la kawaida kwa mchezaji yoyote kuhama timu kutoka moja kwenda nyingine.

“Kuna wakati unaweza ukataka kubaki ndani ya timu moja lakini mambo yakakataa ama ukataka kuondoka na ikawa tofauti ndiyo maisha yetu wanamichezo na ni lazima ukubali matokeo.

“Kikubwa ni kujiamini na kukubali uwezo wako mengine yapo tu ni masuala ya kawaida kwa mchezaji,” amesema.

DAVID SILVA APIGA HESABU ZA KUSEPA NDANI YA MANCHESTER CITY MAJEMBE HAYA SITA YA KAZI YANAPIGIWA HESABU SIMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply