INAELEZWA kuwa Yanga iliyo chini ya Kocha Mkuu, Luc Eymael inawapigia hesabu nyota 10 ili watakaokidhi vigezo watue jumla ndani ya kikosi hicho msimu ujao.
Nyota hao ambao wapo kwenye rada za Yanga ni pamoja na Mussa Mohamed kutoka Nkana, Heritier Makambo anayekipiga Horoya AC, Tuisila Kisinda anayekipiga AS Vita, Michael Sarpong wa Rayon Sports, Yassin Mustapha anayekipiga Polisi Tanzania.
Bakari Mwamnyeto na Ame wote wa Coastal Union, Abdulrahman Humud, Kibwana Shomari na Dickson Job wa Mtibwa Sugar.
Eymael inaelezwa ameacha ripoti ambayo inahitaji kufanyiwa kazi na mabosi wa timu hiyo ya Jangwani.
Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa kwa sasa kazi inayofanyika ni kuwafuatilia wachezaji wote kwa ukaribu kwani dirisha la usajili halijafunguliwa.