Home Uncategorized MABEKI HAWA WAWILI WA SIMBA PASI ZAO ZA MWISHO ZILIMDONDOKEA KAGERE

MABEKI HAWA WAWILI WA SIMBA PASI ZAO ZA MWISHO ZILIMDONDOKEA KAGERE


LICHA ya kuwa ni mabeki Passcal Wawa na Shomari Kapombe ni mitambo ya mabao hawa wawili ndani ya Simba wamehusika kwenye mabao sita ndani ya kosi hilo la mabingwa watetezi.

Shomari Kapombe beki wa pembeni amejaza majalo kwa guu la kulia ambapo pasi yake ya mwisho ilikutana na Meddie Kagere, Uwanja wa Taifa wakati Simba ikishinda mabao 3-2 dhidi ya Azam FC.

Pascal Wawa beki wa kati naye pia pasi ya mwisho alimpa Kagere ilikuwa Uwanja wa CCM Kirumba dhidi ya Alliance ambapo Simba ilishinda mabao 4-1.

Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimama kutokana na janga la Virusi vya Corona na kibindoni Simba imetupia jumla ya mabao 63 na ina pointi 71.

SOMA NA HII  AZAM FC BADO WAMO, LICHA YA KUCHAPWA NJE NDANI NA COASTAL UNION