Uncategorized

CLATOUS CHAMA WA SIMBA AWATAJA WAARABU

admin May 16, 2020 9:28 am
KIUNGO wa Simba, Clatous Chota Chama, amesema kuwa mechi yake bora zaidi ya kimashindano katika ngazi ya klabu ni ile ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly iliyopigwa Februari 12, mwaka jana katika Uwanja  wa Taifa jijini Dar.
Katika mchezo huo, bao pekee lililoipa Simba ushindi liliwekwa kimiani na Meddie Kagere katika dakika ya 65 baada ya kupokea pasi ya John Bocco.Akizungumzia kuhusu maisha ya soka lake la ushindani, Chama raia wa Zambia, amesema:-“Nimecheza michezo mingi katika ngazi ya klabu nikiwa na timu tofauti, lakini kama nitaambiwa nichague mechi moja bora zaidi kati ya zile za ushindani basi ile dhidi ya Al Ahly katika Uwanja wa Taifa ndiyo mechi bora zaidi kwangu.
“Ilikuwa ni mechi ngumu hasa kutokana na ubora wa wapinzani wetu, lakini tulipambana sana kuhakikisha tunaibuka na ushindi na hatimaye tulifanikiwa kuwafurahisha mashabiki wetu.”

Chama ni miongoni mwa nyota ambao walichangia kwa kiasi kikubwa kuifi kisha Simba katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo msimu uliopita.
VIDEO: ISHU YA MSHINDI BSS, MADAM RITHA AFUNGUKA JUMA KASEJA:WACHEZAJI WENGI VIWANGO VITAPOROMOKA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply