Home Uncategorized MO DEWJI FOUNDATION NA KLABU YA SIMBA WASHIRIKIANA KUGAWA BARAKOA 25,000 DAR

MO DEWJI FOUNDATION NA KLABU YA SIMBA WASHIRIKIANA KUGAWA BARAKOA 25,000 DAR



WAKAZI wa maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam, wamekabidhiwa barakoa kwa ajili ya kujilinda na homa kali ya mapafu (COVID-19) inayosababishwa na virusi vya corona.

Ugawaji huo umefanyika leo Jumamosi katika masoko na vituo vya bodaboda ikiwemo maeneo ya Kivukoni, Kariakooo, Tandale, Manzese, Buguruni, Makumbusho, Mabibo, Temeke, Mbagala, Msasani, Kimara, Mbezi na Tegeta.

Barakoa zimekuwa zikishauriwa kutumiwa kama njia ya kupunguza uwezekano wa kusambaza virusi hivyo pale ambapo mtu atakua ana kohoa ama kupiga chafya pamoja na kupunguza umbali ambao maji maji hayo yanaweza kuruka.

Barakoa hizo zimetengenezwa hapa nchini na Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited kwa kutumia pamba inayolimwa hapa nchini. Barakoa hizi ni imara na hivyo kuruhusu uwezekano wa kutumika zaidi ya mara moja baada ya kufuliwa na kupigwa pasi.

Klabu ya Simba imeendelea kuchukua tahadhari kwa kuwalinda wachezaji wake na zoezi hili limekua na lengo la kuwakumbuka wananchi na mashabiki wake pamoja na kuwasihi waendelee kufuata hatua zinazoelekezwa.

Taasisi ya Mo Dewji Foundation imejitolea barakoa hizi ikiwa ni mwendelezo wa kurudisha kwa jamii kwa kuangalia namna bora ambazo inaweza kusaidia katika mapambano dhidi virusi vya corona. Hususani kwa wananchi wa kawaida kuweza kujilinda na kupambana na virusi hivyo.

SOMA NA HII  MK 14 APIGA PICHA NA MCHEZAJI MPYA KIRAKA WA SIMBA KIPENZI CHA MASHABIKI