Home Uncategorized BMT WAANZA MCHAKATO WA KUKUSANYA MAONI KUHUSU UKOMO WA WACHEZAJI WA KIGENI

BMT WAANZA MCHAKATO WA KUKUSANYA MAONI KUHUSU UKOMO WA WACHEZAJI WA KIGENI

BARAZA la Michezo Tanzania, (BMT) limewaomba wadau kuanza kutoa maoni yao kupitia mitandao ikiwa ni pamoja na Facebook, Instagram barua pepe na tovuti kuhusu ukomo wa wachezaji wa kigeni ndani ya Bongo.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Harrison Mw

akyembe alilitoa akiwa bungeni wakati wa kuchangia hoja Kwenye kikao cha bajeti ya mwaka 2020/21.

Mwakyembe alilitaka BMT kuandaa muongozo kuhusu ukomo wa wachezaji wa kigeni kwa kukusanya maoni ya wadau na watu wa michezo.

Taarifa iliyotolewa na BMT kwenda kwa vyombo vya habari imeeleza kuwa kutokana na janga la Virusi vya Corona hawawezi kufanya mkutano hivyo watakusanya maoni kwa njia ya mtandao.

Zoezi la ukusanyaji maoni limeanza Mei 12 mpaka Mei 20 ambapo Ukurasa wao wa Instagram ni nationalsportscouncil_bmt.

SOMA NA HII  HILI NDILO ZOEZI ANALOLIPENDA MBWANA SAMATTA, HAPA NDIPO WALIPO