Home Uncategorized KIFAA MAALUMU CHA MORRISON MAZOEZINI CHAIBUA GUMZO

KIFAA MAALUMU CHA MORRISON MAZOEZINI CHAIBUA GUMZO

BERNARD Morrison nyota wa Yanga amekuwa akifanya mazoezi akiwa amevaa maski maalumu za mazoezi zinazoitwa ‘training mask’ jambo ambalo limemkosha daktari wa timu hiyo Shecky Mngazija.

Wachezaji wa Yanga wameanza mazoezi rasmi kwa ajili ya kujiandaa na mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho.

Mgazija amesema Morrison ni mfano wa kuigwa kwani anafuata maagizo yaliyotolewa kujikinga na Virusi vya Corona.


 “Tuliwapa wachezaji wetu wote maelekezo ya kufanya wanapokuwa mazoezini ili kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona, Morrison amekuwa akifanya kwa asilimia kubwa,” amesema.

SOMA NA HII  KAGERA SUGAR: TUNAWAHESHIMU SIMBA ILA POINTI ZAO TUNAZITAKA PIA