Home Uncategorized MTIBWA SUGAR: TUPO TAYARI KWA AJILI YA KUENDELEA KUPAMBANA

MTIBWA SUGAR: TUPO TAYARI KWA AJILI YA KUENDELEA KUPAMBANA


THOBIAS Kifaru, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya ushindani kutokana na wachezaji wao kuwa na mwendelezo wa mazoezi wakati wa mapumziko yaliyosababishwa na Virusi vya Corona.
Akizungumza na Saleh Jembe,Kifaru amesema kuwa wapo tayari kwa ushindani wakati wowote kutokana na uimara wa falsafa yao na wachezaji makini walionao.
” Tupo tayari kwa ajili ya ligi na kila kitu kipo vizuri kwa sasa ni kufanya maandalizi ya mwisho kabla ya vijana kurudi uwanjani kwani wakati wa mapumziko yaliyosababishwa na janga la Corona vijana walikuwa wanafanya mazoezi.
“Kikubwa ni kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Corona kwani bado janga lipo nasi tutaendelea kuchukua tahadhari ili tuwe salama,” amesema.
Tayari Mtibwa Sugar wameanza mazoezi kwa ajili ya kujiweka sawa ili ligi itakaporejea mambo yaende vizuri.
SOMA NA HII  OLE GUNNAR ANAAMINI RASHFORD NI MATATA KULIKO KANE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here