Home Uncategorized VITA YA KIUNGO ANAYEWINDWA NA YANGA NI DHIDI YA NYOTA WAWILI, DAU...

VITA YA KIUNGO ANAYEWINDWA NA YANGA NI DHIDI YA NYOTA WAWILI, DAU LAKE ACHA


NYOTA Ally Niyonzima anayekipiga ndani ya Rayon Sport ya Rwanda ambaye ni kiungo iwapo dili lake la kutua ndani ya Yanga litajibu basi atakuwa na kazi ya kupambania namba kwa wachezaji wawili wa kazi.

Anatajwa kuwa kwenye rada za mabosi wa Kariakoo ambao ni Mabingwa wa kihistoria ndani ya ligi wakitajwa kuanza kufanya naye mazungumzo kiungo huyo.

Uwezo wake ni kucheza zaidi ya namba mbili uwanjani ila anamudu sana kucheza akiwa namba sita.

Iwapo atatua Yanga vita yake ya namba itakuwa dhidi ya Papy Tshishimbi na Feisal Salum,’ Fei Toto’. Dau lake la usajili linatajwa kuwa milioni 95 ili amwage wino Jangwani.

SOMA NA HII  YANGA YAMVUTIA KASI BEKI WA AS VITA