Home Uncategorized TSHABALALA AFICHUA KILICHO NYUMA YA UBORA WAKE

TSHABALALA AFICHUA KILICHO NYUMA YA UBORA WAKE


MOHAMED Hussein, ‘Tshabalala’ ni mzawa ndani ya kikosi cha mabingwa ambaye amekuwa kwenye ubora wake kwa muda wa misimu mitano alipojiunga na Klabu ya Simba msimu wa 2014.
Tshabalala ni zao la Azam FC ambapo amedumu kuanzaia msimu wa 2014/15, 2015/16,2016/17,2017/18,2018/19 na sasa msimu wa 2019/20. 
Simba ikiwa imefunga mabao 63 amehusika kwenye mabao manne licha ya kuwa ni beki akisema kuwa yote ni kutokana na kujituma kwa ajili ya kuona timu yake inapata matokeo.
Amefunga mabao mawili na kutoa pasi mbili za mabao ambapo mabao yake yote mawili amezifunga timu zenye majina ya Sugar.
Aliwatungua Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba bao lake la kwanza msimu huu kwa pasi ya Meddie Kagere na bao lake la pili aliwatungua Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri kwa pasi ya Jonas Mkude.

Tshabalala amesema kuwa sababu kubwa ya kuwa bora ni juhudi pamoja na kujituma bila kuchoka.
SOMA NA HII  KISA SAFARI YA ZANZIBAR ALLY KAMWE AMPIGA KIJEMBE FEI TOTO