Home Uncategorized BREAKING: CHAMA ATIA TIMU BONGO

BREAKING: CHAMA ATIA TIMU BONGO


KIUNGO wa Simba, Clatous Chota Chama amewasili nchini leo akitokea nchini Zambia alikokuwa kwa ajili ya mapumziko ya lazima yaliyotokana na janga la Virusi vya Corona.

Machi 17 Serikali ilisitisha masuala ya michezo kuendelea kufanyika nchini jambo lililowapa nafasi baadhi ya wachezaji wa Simba akiwemo Chama kuondoka.

Kwa sasa Serikali imeruhusu masuala ya michezo kuendelea nchini huku wakiwataka wadau kuzingatia kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Corona kwa kuwa licha ya maambukizi kupungua bado upo.

Chama ataungana na wachezaji wenzake kambini ambao walianza mazoezi tangu Mei 27 kwenye Uwanja wao uliopo Bunju na mchezo wao wa hivi karibuni ni dhidi ya Ruvu Shooting utakaochezwa Juni 14 Uwanja wa Taifa.

SOMA NA HII  KIGOGO SIMBA AIPA UBINGWA YANGA