Uncategorized

KOCHA WA YANGA AMTAJA MSHAMBULIAJI ATAKAYESEPA BAADA YA MSIMU KUMEGUKA

admin June 12, 2020 9:47 pm


KOCHA wa zamani wa Yanga, Mwinyi Zahera raia wa DR Congo, amefunguka kuwa mshambuliaji wa timu hiyo, David Molinga ataondoka mwishoni mwa msimu huu.

Zahera ambaye kwa sasa yupo nchini Ufaransa ametoa kauli hiyo baada ya kusikia tetesi za mshambuliaji huyo mwenye mabao nane ni miongoni mwa wachezaji wa kimataifa watakaotemwa na timu hiyo katika usajili ujao.
Zahera amesema kuwa kwa upande wake anajua mshambuliaji huyo ataachana na Yanga baada ya kumalizika kwa ligi na Kombe la FA hatokaa kusubiriwa kuachwa kama wengi wanavyofikiria.
“Ninachojua ni kwamba Molinga ataondoka Yanga mwenyewe hatosubiria hadi wao ndiyo watangaze kumuacha kwa sababu yule meneja wake hatoweza kukubali kutokana na kuwepo kwa timu ambazo zitahitaji kuwa naye.
“Unajua yeye wakati huu anasubiria kumalizia mechi ambazo zimebakia kabla ya kuondoka lakini lazima ataondoka mapema bila ya kusubiria mambo hayo ya kuachwa kwa sababu nimekuwa nikiongea naye mara kwa mara,” alisema Zahera.


COASTAL UNION YAZITAKA POINTI TATU ZA NAMUNGO SIMBA YAMALIZANA NA VIUNGO WIWILI WA KAZI FASTA, PESA YATEMBEA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply