Uncategorized

SASA MANCHESTER UNITED YAMGEUKIA BOSI WA SAMATTA

admin June 15, 2020 2:47 pm
MANCHESTER United, inaripotiwa kuwa imeongeza nguvu kubwa kwa sasa kumpata nahodha wa Klabu ya Aston Villa ya Mbwana Samatta, Jack Grealish baada ya kuambiwa kuwa hawatampata Jadon Sancho.
United ilikuwa inahitaji saini ya nyota wa Borussia Dortmund Sancho ila kwa sasa itakuwa ngumu kumpata kwa kuwa Dortmund wamegoma kumruhusu kuondoka kwenye usajili wa majira ya joto Ulaya.
Mabosi wa Dortumud wamewaambia wazi Manchester United kuwa bado wanahitaji huduma ya mchezaji huyo mwenye miaka 20 ambaye amekuwa akiwindwa pia na Liverpool.
Ole Gunnars Solksjaer, Kocha Mkuu wa United inaelezwa kuwa amekubali jina la kiungo wa Aston Villa kuwa mbadala wa Sancho hivyo usajili ambao unapewa kipaumbele kwa sasa ndani ya United ni wa nyota huyo wa Aston Villa anayefanya kazi na Samattta.

IBRAHIM AJIBU MTAMBO WA MABAO MECHI ZA MAZOEZI ILA ZA USHINDANI ANA USHKAJI NA BENCHI MAJEMBE YA KAZI AZAM FC YARUDI KUIWAHI SIMBA, SASA KAZI IPO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply