Uncategorized

ALIYENYOOSHWA NA MWAKINYO TINAMPAY KUKUTANA NA MUZIKI WA MFAUME

admin June 16, 2020 3:47 pm

PROMOTA wa mapambano ya ngumi nchini Juma Msangi maarufu kama Jay Msangi amesema kuwa bondia Mfaume mfaume amesaini mkataba wa kuzichapa na bondia Arnel Tinampay kutoka nchini Thailand.
Tinampay Novemba 2019 alizichapa na bondia Hassan Mwakinyo  ambapo katika pambano hilo alipoteza kwa pointi katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar.
Msangi amesema kuwa tayari bondia mfaume ameshasaini mktaba wa kupigana na bondia huyo hivyo hivi karibuni watatangaza tarehe na mahali pambano litakapofanyika kutokana na kusubiri kibali cha Serikali.
“Kwa sasa tunasubiri kibali cha Serikali kuturuhusu kwa ajili ya mapambano ya ngumi,lakini kuhusu mpambano huo tayari bondia Mfaume ameshasaini mkataba wa kupigana hivyo mambo yakiwa sawa tutangaza mpambano utafanyika lini na sehemu gani,”amesema Msangi.

LACAZETTE PASUA KICHWA, ARSENAL WAKUBALI KUKAA NAYE MEZA MOJA EYMAEL AMPA MASHARTI MATATU MARRISON..LA SIVYO KUISIKIA YANGA KWENYE ‘BOMBA’

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply