Home Uncategorized SIMBA YAINGIA ANGA ZA TP MAZEMBE

SIMBA YAINGIA ANGA ZA TP MAZEMBE

TIMU tatu miamba ya Afrika, TP Mazembe na As Vita za DR Congo na AS Horoya ya Guinea zimeshafuzu Ligi ya Mabingwa Afrika.

Vita na Mazembe zimekuwa zikifanya vizuri kwenye michuano hiyo ambayo kwa Tanzania Simba ndiyo yenye nafasi kubwa ya kufuzu msimu huu.

Horoya ndiyo anayoichezea straika kipenzi cha Yanga, Heritier Makambo ambaye ni raia wa DR Congo maarufu kama ‘Mzee wa Kuwajaza’.

Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kufikia sasa timu ambazo zimeshafuzu ushiriki wa Ligi ya Mabingwa Afrika ni 24.

Lakini ukiondoa Mazembe, Vita na Horoya nyingine zenye rekodi ya kutikisa ni Agosto na Petro de Luanda zote za Angola.

Nchi za Kiarabu zote ikiwamo Algeria, Misri, Tunisia, Morocco bado hatma ya Ligi zao haijafikiwa hivyo hazijatuma wawakilishi.

Kwenye Shirikisho, majina makubwa yaliyofuzu kufikia sasa ni Sagrada Esparanca ya Angola na DC Motema Pembe ya DR Congo.

Mashindano yote msimu ujao yalipangwa kuanza Agosti 7 na kumalizika mwezi Mei lakini huenda yakasogezwa mbele kutokana na janga la corona lililotingisha mataifa mengi duniani.

SOMA NA HII  SIMBA YAKUBALI MAJEMBE YA KAZI YA YANGA