Home Uncategorized PAUL NONGA AGOMEA KUREJEA LIPULI

PAUL NONGA AGOMEA KUREJEA LIPULI


PAUL Nonga, nahodha wa Lipuli amesema kuwa hana mpango wa kurejea kwenye timu kwa sasa mpaka pale watakapokamilisha malipo ya mshahara wake ambao hajalipwa kulingana na mkataba wake.

Nonga hajarejea kambini kwa sasa akiwa amejichimbia Mbeya na familia yake.

Akizungumza na Saleh Jembe, Nonga amesema kuwa Lipuli wamevunja makubaliano ya kwenye mkataba jambo ambalo limemfanya asirejee kambini kwa sasa.

“Kuna makubaliano ambayo tuliyafanya na mabosi zangu Lipuli, kwa kuwa hayajatimizwa sijarejea kambini ili kuungana na wachezaji wenzangu.

“Ninachohitaji kwa sasa ni kuona nalipwa stahiki zangu kwani ni muda mrefu sijapewa haki zangu, nina amini kwamba mambo yakiwa sawa nitarejea kambini,” amesema.

Nonga ni kinara wa utupiaji ndani ya Lipuli akiwa na mabao 11 alikosa mchezo dhidi ya Polisi Tanzania uliochezwa Uwanja wa Ushirika Moshi, ambapo timu zote zilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.

SOMA NA HII  KAZE KUPEWA MIKOBA YA KOCHA WA YANGA