UONGOZI wa Yanga umesema kuwa mpango mkubwa kwenye mchezo wa kesho ni kushinda ili kupata pointi tatu.
Kesho, Juni 24, Yanga itaikaribisha Namungo FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Taifa majira ya saa moja usiku.
Mchezo wa Yanga unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa mchezo wa kwanza waliocheza Uwanja wa Majaliwa, Yanga ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1.
Kwenye mechi zao za hivi karibuni Namungo inayonolewa na Kocha Mkuu, Hitimana Thery ilishinda maao 2-0 mbele ya Kagera Sugar huku Azam FC ikilazimisha sare ya bila kufungana na Azam FC Uwanja wa Taifa.
Timu zoe zina uhakika wa kubaki ndani ya Ligi Kuu Bara kwa kuwa zipo ndani ya tano bora kwa sasa.
Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa wanatambua utakuwa mchezo mgumu ila watapambana kuona wanapata pointi tatu.
Thiery wa Namungo amesema kuwa wamejipanga kucheza mchezo huo mgumu na wanachohitaji ni pointi tatu muhimu.