Home Uncategorized LEO NI VITA YA UBINGWA, SIMBA NA YANGA WOTE WANAKIWASHA UWANJANI

LEO NI VITA YA UBINGWA, SIMBA NA YANGA WOTE WANAKIWASHA UWANJANI


HESABU za mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara kuweza kufikia malengo ya kutwaa ubingwa itaanza kuhesabiwa leo iwapo itashinda mchezo wake dhidi ya Mbeya City picha kamili ya ubingwa itaanza kuonekana.
Iwapo Simba itashinda leo itabakiza mechi mbili ili kutangazwa kuwa mabingwa wa Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2019/20 kwa kuwa imecheza mechi 30 na pointi zake 75 ikishinda mechi tatu mfululizo itafikisha jumla ya pointi 84 ambazo hazitafikiwa na timu yoyote.
Wapinzani wake wakubwa ni Azam na Yanga ambao nao pia wanacheza leo na wote  wamebakiza mechi nane baada ya kucheza mechi 30 ambazo ni sawa na pointi 24 ambapo Azam FC iliyo nafasi ya pili ina pointi zake 58 ikishinda mechi zote itafikisha pointi 82 huku Yanga yenye pointi 56 ikiwa nafasi ya tatu ikishinda mechi zote itafikisha pointi 80.
Mechi zote tatu zitakuwa ni za kukata na shoka, Mbeya City iliyo chini ya Kocha Mkuu, Amri Said itaingia uwanjani ikiwa na hesabu za kulipa kisasi ya kichapo walichokutana nacho Novemba 11, Uwanja wa Uhuru, kwa kufungwa mabao 4-0 wakati huo Mbeya City ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Juma Mwambusi.
Uongozi wa Mbeya City,iliyo nafasi ya 18 na pointi 30 kupitia Ofisa Habari wao, Shaha Mjanja umeliambia Championi Jumatano kuwa kila kitu kipo sawa na wanahitaji kupata ushindi ili kujinusuru kushuka daraja.
Sven Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba alisema kuwa wachezaji wake wapo tayari kwa ushindani na kikubwa wanachohitaji ni pointi tatu ndani ya uwanja.
Mchezo mwingine mkali ni dhidi ya Yanga iliyo chini ya Kocha Mkuu, Luc Eymael dhidi ya Namungo FC, iliyo nafasi ya nne na pointi 54 ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Hitimana Thiery, Uwanja wa Taifa majira ya saa 1:00 usiku.
 Mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Majaliwa timu zote zilitoshana kwa kufungana bao 1-1.Mechi zao za hivi karibuni, Yanga ililazimisha sare ya bila kufungana na Azam FC Uwanja wa Taifa, huku Namungo ikishinda mabao 2-0 mbele ya Kagera Sugar Uwanja wa Majaliwa.
Eymael ameliambia Championi Jumatano kuwa wachezaji wake wapo tayari kwa ajili ya mechi zote zilizobaki kupata pointi tatu muhimu.Thiery wa Namungo alisema kuwa watapambana kupata ushindi kwenye mchezo wao mgumu dhidi ya Yanga.
Balaa lingine litakuwa Uwanja wa Kaitaba ambapo Kagera Sugar itamenyana na Azam FC, Uwanja wa Kaitaba, majira ya saa 10:00.Kagera Sugar iliyo chini ya Kocha Mkuu, ikiwa na pointi 41, Mecky Maxime mchezo wake wa mzunguko wa kwanza , Uwanja wa Chamazi, Novemba 4,2019 ililazimisha sare ya bila kufungana na Azam FC hivyo leo kazi itakuwa nzito kwa Kocha Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba kusaka pointi tatu.
SOMA NA HII  MSHAMBULIAJI WA YANGA APANIA KUFANYA MAKUBWA, KIWANGO CHAKE ADAI HAKIJAMFURAHISHA