MASHABIKI wa timu ya Ndanda FC, jana, Juni 27, hawajaamini wanachokiona ndani ya Uwanja wa Taifa baada ya Yanga kupindua meza kibabe kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliokuwa na ushindani mkubwa.
Yanga ilianza kufunga bao la kwanza dakika ya sita kupitia kwa Deus Kaseke ambalo liliwekwa sawa na Abdul Hamis aliyepachika bao la kwanza kwa Ndanda FC dakika ya 10 na wakaongeza la pili dakika ya 16 kupitia kwa Omary Mponda.
Dakika ya 45, Kaseke aliweka mzani sawa na kufanya matokeo iwe 2-2 mpaka muda wa mapumziko jambo liliwafanya mashabiki wa Ndanda waamini kwamba watagawana pointi mojamoja.
Kipindi cha pili Yanga walianza kwa kasi baada ya kuingia kwa Mrisho Ngassa dakika ya 64 akichukua nafasi ya Ditram Nchimbi na aliongeza bao la tatu na la ushindi dakika ya 73.

Bao hilo la Ngassa, liliwafanya mashabiki wa Ndanda kupoteza matumaini ya kusepa na pointi moja kwa Yanga ambayo ilikuwa ikishambulia lango la Ndanda kwa kasi.
Ushindi huo unaifanya Yanga kuishuhusha Azam FC nafasi ya pili baada ya kufikisha pointi 60 huku Azam FC ikiwa nafasi ya tatu na pointi zake 59 zote zimecheza mechi 32.