Home Uncategorized BUMBULI WA YANGA AFUNGUKIA UHUSIANO WAKE NA HAJI MANARA WA SIMBA

BUMBULI WA YANGA AFUNGUKIA UHUSIANO WAKE NA HAJI MANARA WA SIMBA


HASSAN Bumbuli, Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga amesema kuwa wana mahusiano ya ukaribu kikazi na Ofisa Habari wa Simba Haji Manara.
Bumbuli anasimamia kitengo cha Habari ndani ya Klabu ya Yanga ambapo mpinzani wake mkubwa ni Haji Manara anayesimamia kitengo cha Habari cha Simba. 
Mabosi hawa wamekuwa wakitumiana maneno kwa kila mmoja kulinda nembo ya timu yake kwa wakati wake.
Bumbuli amesema kuwa:“Uhusiano wetu na Haji Manara upo,sawa kwenye masuala ya kikazi licha ya kuwa huwa kunaotkea tofauti za hapa na pale.
“Ipo wazi katika hilo hasa tunapokuwa kwenye kazi, ila naona yeye anataka kuwashambulia wenzio ila yeye hataki, hiyo sio sawa lazima akubaliane na hali halisi kwani ukiwa unashambulia nawe ni lazima ukubali kushambuliwa.”
SOMA NA HII  YANGA YATAMBA KUPATA DAWA YA SARE, KAZI KUANZA KESHO TAIFA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here