KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Hassan Dilunga, amewaomba mashabiki wao kuifuata timu popote itakapokabidhiwa Kombe la Ligi Kuu Tanzania Bara.
Simba wamefanikiwa kutetea ubingwa wao kwa mara ya tatu mfululizo wakiwa bado wana michezo sita mkononi baada ya juzi kutoka suluhu na Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya.
Akizungumza jana kupitia mtandao wa kijamii wa Klabu ya Simba, Dilunga alisema amefurahi kuwa mabingwa kwa mara nyingine.
Dilunga alisema pamoja na kutwaa ubingwa wa msimu huu, hawajui wapo watakabidhiwa kombe hilo, hivyo kuwaomba mashabiki kuifuata timu popote itakapokabidhiwa.
Alisema wataendelea kutwaa ubingwa kwa misimu ijayo mfululizo ili waweze kuiwakilisha nchi katika michuano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
“Tunafuraha sana na tunaahidi kuendelea kuchukua kombe mfululizo,”alisema Dilunga.
Simba wamefanikiwa kutetea taji hilo, baada ya kufikisha pointi 79, ambazo hazitafikiwa na timu nyingine zinazoshiriki ligi hiyo.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.