Home Uncategorized HIVI NDIVYO AZAM FC ILIVYONYOOSHWA NA SIMBA DAKIKA 450

HIVI NDIVYO AZAM FC ILIVYONYOOSHWA NA SIMBA DAKIKA 450


USHINDI wa mabao 2-0 walioupata Simba mbele ya Azam FC, juzi Uwanja wa Taifa unaifanya Azam FC ikubali kupoteza jumla ya mechi tano ambazo ni sawa na dakika 450 mbele ya timu hiyo.

Mabao ya Simba yalifungwa na John Bocco na Clatous Chama ambayo yanaipa tiketi ya kutinga hatua ya nusu fainali na watakutana na Yanga ambayo ilishinda mabao 2-1 mbele ya Kagera Sugar, Uwanja wa Taifa.
Mechi ambazo walikutana nao ndani ya msimu wa mwaka 2019/20 ulikuwa wa kwenye ngao ya jamii ambapo Azam FC ilikubali kufungwa mabao 4-2.
Kwenye mechi mbili za Ligi Kuu Bara, Simba ilishinda mechi zote ambapo ule wa kwanza walishinda bao 1-0 na wa pili walishinda mabao 3-2. Walipokutana visiwani Zanzibar hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho, Simba ilishinda kwa penalti 3-2 baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya bila kufungana.
Ndani ya dakika 450, Azam FC imefungwa jumla ya mabao 10 huku ikiwa imefunga mabao manne.
SOMA NA HII  KATWILA: DIRISHA DOGO TUTAFANYA USAJILI UTAKAOTUBEBA