MSHAMBULIAJI namba moja wa Klabu ya Mwadui FC Gerald Mathias Mdamu amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya KMC utakaochezwa Uwanja wa Uhuru.
Mdamu ametupia mabao matano na kutoa pasi tatu za mabao ndani ya Mwadui FC ambayo imefunga jumla ya mabao 31.
Akizungumza na Saleh Jembe, Mdamu amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mechi hiyo wanaamini watapata pointi tatu muhimu.
“Tupo kwenye vita kwa sasa hivyo hatuna kingine tunachokitafuta ndani ya uwanja zaidi ya pointi tatu muhimu.
“Nafasi ambayo tupo bado haitufurahishi kwani ushindani ni mkubwa na kila timu inakazana kupata ushindi ni jambo la kusubiri na kuona namna gani tunaweza kuibuka na ushindi kwani wapinzani wetu tunawaheshimu,” amesema.
Mwadui ipo nafasi ya 12 ikiwa imejikusanyia pointi 40 inamenyana na KMC iliyo nafasi ya 15 na pointi zake 37 zote zimecheza mechi 32.