Home Uncategorized YANGA YAPIGA HESABU KUWEKA REKODI MPYA KARUME LEO

YANGA YAPIGA HESABU KUWEKA REKODI MPYA KARUME LEO


YANGA iliyo chini ya Kocha Mkuu, Luc Eymael leo imepanga kuweka rekodi mpya ya kupata kusepa na pointi tatu mbele ya Biashara United, Uwanja wa Karume.
Yanga haina bahati ya kushinda kwenye Uwanja wa Karume ndani ya dakika 90 kwani msimu uliopita ilipokutana kwa mara ya kwanza na timu hiyo ikiwa imepanda daraja msimu wa 2018/19 iliyeyusha pointi zote tatu kwa kuchapwa bao 1-0.
Akizungumza na Saleh Jembe, Eymael amesema kuwa kuna ugumu wa kupata matokeo kwenye mechi yake hiyo kutokana na ubovu wa sehemu ya kuchezea ila anahitaji ushindi.
“Ni ngumu kwa sasa kusema kwamba tutashinda ila kikubwa ni kwamba tunahitaji ushindi na pointi tatu ni muhimu kwetu licha ya kwamba uwanja ni kikazo namba moja kwetu,” amesema Eymael.  
Yanga imekutana na Biashara United mara tatu kwenye mechi za ligi tangu msimu wa 2018/19, Yanga ilishinda mchezo mmoja wa Novemba 29 kwa mabao 2-1, Uwanja wa Taifa na ilipoteza mchezo uliochezwa Mei 10 Uwanja wa Karume kwa kufungwa bao 1-0.
Mchezo wa tatu msimu huu, Yanga ilishinda bao 1, hivyo ndani ya dakika 270, Yanga imeifunga Biashara United mabao matatu na imefungwa mabao mawili, huku kwenye pointi tisa ikikomba sita na kuyeyusha pointi tatu.
Ikiwa nafasi ya pili na pointi 60  itakuwa na kazi ya kutafuta pointi tatu kwa Biashara United iliyo nafasi ya tisa na pointi 44 zote zikiwa zimecheza mechi 32.
SOMA NA HII  SIMBA YATAKA KUBEBA MATAJI MAKUBWA MAWILI