MCHEZO wa Ligi Kuu Bara uliochezwa jana, Uwanja wa Azam Complex kati ya Azam FC v Singida United ulikamilika kwa Azam FC kuishushia mvua ya mabao Singida United.
Mpaka dakika 90 zinakamilika Azam FC kibindoni ilikuwa imefunga mabao 7-0 dhidi ya Singida United ambayo imeshashuka daraja.
Huo ni ushindi mkubwa kwa Azam FC msimu huu ambapo mchezo mwingine walioshinda mabao mengi ulikuwa dhidi ya Alliance FC ambapo ilishinda mabao 5-0.
Mshambuliaji Obrey Chirwa alisepa na mpira baada ya kufunga hat trick na kuongeza bao moja na kufanya afunge jumla mabao manne na kufikisha mabao 12 kibindoni.
Azam FC inafikisha pointi 62 na kuishusha Yanga nafasi ya tatu Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mvua ya mabao ilianza kupitia kwa Idd Seleman ‘Naldo’ aliyefunga mawili dk ya 2 na 13 huku Natley wa Singida United akijifunga dk 41, Chirwa alifunga dk 44,55,56 na 62.
Azam FC imebakiza mechi tano kukamilisha mzunguko wa pili baada ya kucheza mechi 33.
Kwa upande wa vita ya ufungaji bora inazidi kupanda joto kati ya Meddie Kagere wa Simba mwenye mabao 19 na Yusuph Mhilu wa Kagera Sugar mwenye mabao 13.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.