KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison leo alitumia dakika 64 ndani ya Uwanja wa Taifa huku akidhibitiwa na mabeki wa safu ya Simba iliyokuwa ikiongozwa na Pascal Wawa kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya nusu fainali.
Baada ya Morriosn kutolewa aligoma kukaa benchi na wachezaji wenzake jambo ambalo lilizua taharuki licha ya kurudishwa na mwamuzi wa nje hakutaka kufanya hivyo zaidi ya kuongeza mwendo kuelekea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.
Nafasi ya Morriosn ilichukuliwa na Patrick Sibomana ambaye aliongeza kasi ya mashabulizi kwa Simba na kubadilisha upepo kwa kiasi chake baada ya kuingia uwanjani.
Yanga ilitinga hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Kagera Sugar mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa.
Kufungwa leo mbele ya Simba kumeyeyusha matarajia ya timu hiyo kushiriki michuano ya kimataifa hivyo wana kazi ya kujipanga msimu ujao.
Mchezo wa leo Simba imeshinda mabao 4-1 na unawapa tiketi ya kusonga hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho ambapo watacheza na Namungo FC ya Lindi.
Fainali inatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga ambapo bingwa wa msimu uliopita alipatikana Uwanja wa Ilulu ambaye ni Azam FC.
Azam FC ilitolewa na Simba hatua ya nusu fainali kwa kufungwa mabao 2-0 mchezo ulichezwa Uwanja wa Taifa.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.